Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katika siku ya mazingira duniani dunia itasherehekea thamani ya misitu:UNEP

Katika siku ya mazingira duniani dunia itasherehekea thamani ya misitu:UNEP

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP limesema iwe ni kufanya usafi karibu na mlima Everest, mpango wa mafunzo ya utunzaji misitu Costa Rica au tamasha la muziki Ubelgiji, mamilioni ya watu wataungana Juni 5 kuadhimisha siku ya kimataifa ya mazingira.

Kauli mbiu mwaka huu ni ‘misitu huduma ya mali asili kwa ajili yako”, ambayo itatanabahi umuhimu wa mazingira, uchumi na jukumu la kijamii linalobebwa na misitu duniani.

Kimataifa sherehe za mwaka huu zitafanyika India ambako kutakuwa na matukio mbalimbali mjini Delhi na Bangalore ikiwemo mashindano ya ridha ya kilometa 10 yakijumuisha wakimbiaji 2500. George Njogopa anaripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)