2 Juni 2011
Watu takribani bilioni 5 watakuwa wanaishi katika miji mikubwa duniani ifikapo mwaka 2030. Wengi wao watakuwa ni wahamiaji wa makundi ya walio wachache ambao watakuwa wakitafuta fursa za uchumi na uhuru.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema dunia inaweza kupata funzo zuri kutoka Italia ambayo imekuwa mpokeaji wa wahamiaji na pia taifa la wahamiaji.Ban ameyasema hayo mjini Roma Italia alikohudhuria mkutano wa kimataifa kuhusu mji wenye watu mchanganyiko wa sehemu mbalimbali.
(SAUTI YA BAN KI-MOON)
Ban pia amehudhuria hafla ya miaka 150 ya muungano wa Italia na kukutana na maafisa mbalimbali wa serikali.