Majeshi ya serikali na wapinzani libya wametekeleza uhalifu wa kivita

2 Juni 2011

Jopo la Umoja wa Mataifa lililopewa jukumu la kuchunguza ukiukaji wa haki za binadamu nchini Libya limesema majeshi ya serikali na upinzani wote wamefanya uhalifu wa kivita katika wiki zilizoghubikwa na mapigano kufuatia machafuko ya kupinga uongozi wa Rais Kanali Muammar al-Gadhafi.

Jopo hilo lililo na wajumbe watatu wa kimataifa lililotumwa na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limewasilisha ripoti ya matokeo ya uchunguzi wake kwa wajumbe 47 wa baraza hilo mjini Geneva hii leo. Ripoti hiyo imekuja huku kukiwa na hofu kubwa ya kuendelea kuzorota kwa hali ya kibinadamu katika taifa hilo la Afrika Kaskazini ikiwa ni pamoja na matatizo ya chakula, huku juhudi za kidiplomasia za kumaliza mzozo huo zikiendelea. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter