Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Unicef watoa wito wa ukiukaji wa haki za watoto somali

Unicef watoa wito wa ukiukaji wa haki za watoto somali

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limetanabaisha kile ilichoeleza kwamba ni ukiukaji mkubwa wa haki za watoto unaokufa kila siku nchini Somalia, taifa lililoghubikwa na vita tangu kupinduliwa serikali miaka 20 iliyopita.

Katika taarifa yake iliyotolewa leo UNICEF imesema watoto katika eneo la katikati mwa Somalia wanakabiliwa na mateso na manyanyaso yasiyokwisha , wakizongwa na ghasia kila siku ambazo zinaweka maisha yao katika hatari ya kuuawa, kujeruhiwa au hata kupewa mafunzo na kutimiwa vitani na pande zote zinazohusika katika vita vya Somalia.

Shirika hilo limeongezza kuwa asilimia 46 ya watoto waliopelekwa hospitali mwezi uliopita mjini Moghadishu wana majeraha yatokanayo na risasi au kuungua , taarifa ambazo pia zimetolewa na shirika la afya duniani WHO.