Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maafisa wa ngazi za juu jeshini nchini Libya waliasi jeshi

Maafisa wa ngazi za juu jeshini nchini Libya waliasi jeshi

Majenerali nane kwenye jeshi la Libya wameliasi jeshi hilo na kutoa wito kwa wenzao kuungana nao. Majenerali hao pia wametoa wito wa kusitishwa kwa dhuluma zinazoendeshwa dhidi ya raia Libya huku madai yakisema kuwa zaidi ya maafisa 100 wameihama nchi hiyo.

Akilihutubia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa naibu Katibu Mkuu katika masuala ya kisiasa Lynn Pascoe anasema kuwa waasi kwa sasa wanaudhibiti mji ulio mashariki wa Misrata. Pascoe anasema kuwa uasi jeshi unazidi kuongezeka kwenye jeshi la Libya wakiwemo majenerali nane ambao kwa sasa wako nchini Italia na maafisa wengine wengi.