Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sri Lanka ifanye uchunguzi wa mauaji: Hynes

Sri Lanka ifanye uchunguzi wa mauaji: Hynes

Mtaalamu wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa utawala nchini Sri Lanka kuchunguza mauaji ya wanaume kadha yaliyotekelezwa na jeshi. Christof Heyns mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayeshughulika na mauaji yanayofanywa kinyume na sheria aliyataja mauaji yaliyoonyesha kwenda kanda ya video na yanayopingwa na serikali ya Sri Lanka kama mfano tu wa mauaji yanayofanywa kinyume na sheria.

Kwenye kanda ya video iliyo na picha zilizopeperushwa mara ya kwanza kwenye kituo kimoja cha runinga nchini Uingereza wanaume walio uchi  waanaonekana mikono ikiwa nyumma kabla ya kupigwa risasi. Bwana Heynes anasema kuwa hii inaonyesha kwa mauaji haya yalitekelezwa na ni lazima yachunguzwe zaidi kubaini nani aliyatekeleza.