Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana 2500 wanaambukizwa HIV kila siku:UM/ Banki ya dunia.

Vijana 2500 wanaambukizwa HIV kila siku:UM/ Banki ya dunia.

 

Kila siku inakadiriwa kuwa vijana 2500 wanapata maambukizi mapya ya HIV kwa mujibu wa ripoti ya kimataifa kuhusu kuzuia maambukizi ya HIV iliyozinduliwa leo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo wakati maambukizi yamepungua kiasi miongoni mwa vijana, wasichana na vigori wanakabiliwa na hatari ya maambukizi kwa sababu za kibaolojia, kutokuwepo usawa na kutengwa. Kwa mara ya kwanza ripoti hiyo “fursa katika migogoro:kuzuia HIV kuanzia kwa umri mdogo hadi ujanani, inatoa takwimu kuhusu maambukizi miongoni mwa vijana na kubainisha hatari inayowakabiri wakati wakielekea utu uzima. Jason Nyakundi anaripoti:

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)