Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Simu za mikononi zinasababisha hatari ya kupata saratani:WHO

Simu za mikononi zinasababisha hatari ya kupata saratani:WHO

Ushahidi mpya unaonyesha kwamba simu za mkononi zinaweza kuongeza hatari ya kupata saratani ya ubongo. Kituo cha utafiti wa saratani cha shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO kimetaja rasmi aina ya mionzi inayotolewa na simu za mkononi ambayio inaweza kusabbabisha saratani.

Utafiti wa WHO umebaini kwamba kuna ongezeko la asilimia 40 la hatari ya kupata glioma aina ya saratani ya ubongo kwa watu wanaotumia simu za mkononi kwa takribani dakika 30 kwa siku kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi. Dr Jonathan Samet ni mwenyekiti wa jopo la kimataifa la wataalamu mjini Lyon Ufaransa ambao walitathimini ushahidi huo.

(SAUTI YA DR JONATHAN SAMET)