Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM washerehekea miaka 50 ya teknolojia ya anga za mbali

UM washerehekea miaka 50 ya teknolojia ya anga za mbali

Umoja wa Mataifa unasherehekea miongo mitano ya maendeleo yaliyopigwa katika anga za mbali. Leo unaadhimisha miaka 50 tangu binadamu wa kwanza kufanya safari kwenye anga za mbali ambaye ni marehemu Yuri Gargarin kutoka Urusi aliyezunguka anga hiyo.

Tangu wakati huo kamati ya kudumu ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya matumizi ya amani ya anga za mbali imepitisha mikataba mitano ya kuongoza na kudhibiti matumizi ya anga za mbali. Pia imezisaiodia nchi kujijengea uwezo wa matumizi ya teknolojia ya anga kwa maendeleo amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon katika ujumbe maalumu wa siku hii.

Baadhi ya vifaa vinavyotumik kila siku ni satellites kwa ajili ya mawasiliano, mifumo ya kuongoza safari na teknoloji ya kudadisi masuala ya dunia. Teknolojia ya anga za mbali pia imesaidia katika utabiri wa hali ya hewa, kulinda amazingira na misaada ya kibinadamu.