Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za binadamu hazitekelezwi hata wakati wa matatizo:UM

Haki za binadamu hazitekelezwi hata wakati wa matatizo:UM

Upunguzaji usio wa msingi wa matumuzi yaliyowekwa kutekeleza huduma za jamii ambazo ni muhimu kwa haki za kiuchumi, kijamii na kitamaduni itakuwa ni ukiukaji wa viwango vya haki za binadamu ameonya mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa Magdalena Sepulveda wakati akiwasilisha ripoti yake kuhusu haki za binadamu na umasikini uliokithiri kwenye baraza la haki za binadamu hii leo.

Amesema haki za binadamu hazizingatiwi wakati wa matatizo na kujenga upya mataifa baada ya migogoro. Amesema hata kama kuna matatizo ya fedha serikali zinapaswa kisheria kuheshimu , kuwalinda na kutimiza wajibu wake wa kutekeleza haki za binadamu.

Mtaalamu huyo ameonya kwamba hatua nyingi za kuchipua uchumi zilizochokukuliwa na mataifa mbalimbali zinatishia utekelezaji wa haki za kiuchumi, kijamii na kitamaduni hasa kwa watu masikini na makundi yanayohitaji msaada. Amezitaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kupunguza ulizi wa msaada wa kijamii, kuongeza kodi, na kufuta mgao wa chakula hasa kwa watu masikini ambao wanaishi kwa kutegemea mgao huo, na kusema kufanya hivyo kuna athari kubwa za haki za binadamu.