Ban ametua mwanadiplomasia mzoefu kusimamia timu ya usimamizi wa mabadiliko

1 Juni 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua afisa wa ngazi za juu kwenye umoja huo ambaye atahusika na ufutiliaji wa agenda muhimu inayotaka kufanyika mageuzi ndani ya chombo hicho.

 Ban amesema amemteua mwanadiplomasia Atul Khare ambaye ataongoza timu ya usimamizi wa mabadiliko na atafanya kazi kwa kushirikiana na nchi zote wanachama wa umoja huo zipatazo 192 pamoja na mashirika yote ya Umoja wa Mataifa.

 Akitangaza uteuzi huo Ban amesema kuwa timu hiyo itakuwa na kazi kubwa ya kusimamia mchakato wa mageuzi ndani ya umoja huo na itafanya kazi kwa kuangazia maeneo yote muhimu huku ikihakikisha kwamba mageuzi hayo yanafanyika kwa ufasaha na weledi mkubwa.

Timu hiyo ambayo itafanya kazi kwa usimamizi wa karibu wa Naibu Katibu Mkuu Asha-Rose Migiro inatizamwa kama shabaya ya makusudi ya Umoja wa Mataifa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter