Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bob Geldof atembelea ukanda wa Gaza

Bob Geldof atembelea ukanda wa Gaza

Mwanamuziki mashauri wa rock ambaye amejifungamanisha katika kampeni za kutetea wanyonge ametembelea katika eneo la ukingo wa Gaza ambako ameelezea hali ngumu inayowandama mamia ya watoto kwenye eneo hilo.

Bob Geldof ambaye ametembelea kambi moja inayowahifadhia wakimbizi ya Jabala iliyoko Kaskazini mwa Gaza amesema kuwa hata hivyo watoto kwenye eneo hilo bado wanatoa sura ya matumaini.

Mwanamziki huyo alikuwa safarini kulekea mjini Tel-Aviv kwa ajili ya kuhudhuria mkutano maalumu ulioandaliwa na Israel kwa ajili ya Afrika. Amesema akiwa safarini alipokea mwaliko uliomwomba kwenda kwenye kambi hiyo na hivyo bila kusita alikubali kufanya hivyo.