Vijana wengi Misri wanataka kuondoka nchini humo:IOM

31 Mei 2011

Utafiti uliofanywa na shirika la umoja wa mataifa linalohusika na uhamiaji IOM  nchini Misri,umebainisha kuwa vijana wengi nchini humo bado wanashauku ya kwenda sehemu nyingine lakini hata hivyo mabadiliko ya kisiasa yaliyojotokeza hivi karibuni yanawatatiza kufia maumuzi ya moja kwa moja.

Utafiti huo ambao umewahusu vijana kadhaa umeonyesha kuwa jambo kuu linalowasukuma vijana hao ni kutokana na kukosekana kwa nafasi za ajira, kutokuwepo kwa uhakika juu ya hali ya usalama na kushuka kwa ubora wa maisha.

Pamoja na kwamba kumejitokeza kwa kundi Fulani la vijana ambalo limebadili msimamo wa uhamiaji katika nchi nyingine kufuatia mabadiliko ya kisiasa ya mwezi January, lakini hata hivyo bado kundi kubwa la vijana linaendelea kushikilia shauku ya kutimiza ndoto zao za kuhama.

Mwakilishi wa IOM katika eneo la mashariki ya kati Pasquale Lupoli,amesema kuwa wasiwasi mkubwa unaojitokeza sasa kwa vijana wengi ni kuhusu nafasi za ajira, ikiwa ndani ya nchi yao Misri ama kwingineko duniani.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud