UM waipongeza Ghana kwa huduma za afya

31 Mei 2011

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za kuwa na afya Anand Grover ameipongeza serikali ya Ghana kutokana na kujitolea kwake katika kuwahakikishia wananachi wake haki ya afya.

Akikamilisha ziara yake nchini humo mjumbe huyo hata hivyo amesema kuwa kuna changamoto nyingi hasa katika upande wa afya.

Grover amasema kuwa kazi uliofanya utawala wa nchi hiyo katika kuimarisha sekta zake za kiafya na kuhakikisha kuwa kila mmoja amepata huduma za afya na pia kuboresha huduma za bima ni ya kutia moyo.

Lakini hata hivyo ameseema kuwa inastahili kayatilia maanani maeneo ambayo inatoa huduma hizo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud