Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwongozo kuhusu biashara na haki za binadamu watolewa

Mwongozo kuhusu biashara na haki za binadamu watolewa

Mwongozo ambao umekuwa ukisubiriwa kwa muda kuhusu biashara na haki za binadamu hatimaye umewasilishwa na mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na biashara na haki za binadamu John Ruggie wakati wa kikao cha baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa.

Mwongozo huo una lengo la kuweka viwango vya kimataifa kwa mara ya kwanza vya kuzuia na kushughulikia athari za haki za binadamu zinazohusina na shughuli za kibiashara.

Mwongozo huo umeundwa kutokana na kujumuishwa pamoja kwa maoni , kufanywa ziara kwa zaidi ya nchi ishirini , mawasiliano ya mtandao yaliyowavutia maelfu ya watu kutoka karibu nchi 120 pamoja na mchango kutoka kwa wataalamu kote duniani.