Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi ya tumbaku bado yako juu:WHO

Matumizi ya tumbaku bado yako juu:WHO

Katika siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya tumbaku, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon amesema mwaka huu iimeangukia wakati wa maandalizi ya mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa utakaofanyijka Septemba kuhusu magonjwa yasoto ya kuambukiza.

Na amesema kwa kudhibiti matumizi ya tumbaku itasaidia kushughulikia magonjwa mengi sugu yasiyo ya kuambukiza kama saratani na maradhi ya moyo.

Amesema matumizi ya tumbaku yanachangia vifo vingi, huku takwimu zikionyesha katika karne ya 21 pekee watu milioni 100 wakekufa, na ameonya endapo hatua hazitochukuliwa sasa basi takribani watu bilioni moja wanaweza kufariki dunia kwa maradhi hayo karne hii.

Amesema hatua zinazopaswa kuchukuliwa ni kuanzia kupunguza mahitaji kwa kuongeza bei na ushuru hadi kudhibiti matangazo na udhamini, kuweka tahadhari kwenye paketi za sigara, na kutowauzia watoto na kufikisha ujumbe kwamba matumizi ya tumbaku yanazidisha umasikini hasa katika afya na uchumi.

Nalo shirika la afya duniani WHO linasema watu milioni sita wanaweza kufa mwaka huu kwa maradhi yatokanayo na tumbaku, wakiwemo laki sita ambao sio watvutaji wa tumbaku.

WHO pia imepongeza juhudi za kukabili matumizi ya tumbaku kwa zaidi ya nchi 172, duniani lakini limesisitiza juhudi zaidi zinahitajika. Dr Nyo Nyo Kiang ni mshauri kuhusu masuala ya tumbaku kwenye shirika la WHO anasema nchi zinazoendelea zinajivuta kuchuklua hatua za kudhibiti matumizi ya tumbaku.

(SAUTI YA DR NYO NYO KIANG)

Nao baadhi ya watu kutoka katika nchi hizo zinazoendelea wana maoani wana maoni haya kuhusu siku hii?

(SAUTI MAONI KENYA)