Mamia ya watu wanaendelea kukimbia machafuko Abyei

31 Mei 2011

Watu takribani 60,000 wamelazimika kukimbia kwenye jimbo lenye kuzozaniwa na Abyei nchi Sudan kutokana na mchafuko yanayoendelea umesema Umoja wa Mataifa.

Operesheni kubwa za kibinadamu zinaendelea hivi sasa ili kuwafikia wakimbizi wa ndani , lakini zimekuwa zikikabiliwa na vikwazo kutokana na hali ya usalama, mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na upungufu wa mafuta Sudan kusini.

Ofisi ya Umoja wa mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA imesema juhudi za misaada ya kibinadamu pia zinakabiliwa na ugumu wa eneo kubwa ambako watu wamekimbia na wengi bado wamejificha porini.

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linasema hadi leo limeandikisha wakimbizi wa ndani 30,642 kutoka Abyei, wengi wakiwa wanawake, watoto na wazee na linawafuatilia wengine 30,000 kwa ushirikiano na shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Adrian Edward ni kutioka shirika la UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

Nalo shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema linatarajia eneo hilo kukabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula katika miezi ijayo kwa kuwa watu wanakimbia machafuko kaatia msimu wa kupanda jimboni humo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud