Pillay alaani matumizi ya nguvu dhidi ya waandmanaji Yemen

31 Mei 2011

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay leo Jumanne amelaani matumizi makubwa ya nguvu dhidi ya waandamanaji wanaopinga serikali nchini Yemen ambayo yamedaiwa kusababisha vifo na majeruhi wengi katika siku chache zilizopita.

Pillay amesema ofisi ya haki za binadamu imepokea taarifa ambazo zinasubiri kuthibitishwa kwamba zaidi ya watu 50 wameuawa na jeshi la serikali ya Yemen, vikosi vya ulinzi vya Republican Guards na watu wengine wanaohusiana na serikali tangu Jumapili mjini Taiz.

Vifovimetokea wakati ambapo walisambaratisha kundi la waandamanaji waliokusanyika Horriya Square kwa kutumia mipira ya maji, vifaru na risasi, mamia wengi wamejeruhiwa. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud