Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM/WFP wanawasaidia wahamiaji Misrata

IOM/WFP wanawasaidia wahamiaji Misrata

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP wanashirikiana kuwasaidia mamia ya wahamiaji waliokwama Misirata Libya.

IOM Jumatatu jioni imefanya tena safari ili kuliahamisha kundi lililosalia la wahamiaji . Mamia kadhaa ya wahamiaji wanakadiriwa kusalia Misrata wakisubiri msaada wa kuhamishwa ikiwa ni pamoja na raia wa Libya ambao wamejeruhiwa.

WFP kwa kutumia meli hiyo ya IOM imepeleka tani 500 za chakula Misrata ikiwa ni pamoja na unga wa ngano, mafuta ya kupikia na biskuti. Mashariki mwa Libya WFP imeweza kuwafikishia msaada wa chakula zaidi ya watu 250,000 na Magharibi mwa nchi hiyo watu 29,000 wameshapata msaada.

Lakini imeshiondwa kuwafikia watu wa jimbp la Magharibi la milimani kutokana na usalama mdogo na upungufu wa mafuta.