Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wengi wanajeruhiwa Somalia:WHO

Watoto wengi wanajeruhiwa Somalia:WHO

 

Shirika la afya duniani WHO linasema kumekuwa na ongezeko la idadi ya watoto wanaojeruhiwa katika machafuko nchini Somalia. Kwa mujibu wa shirika hilo katika mwezi mmoja uliopita katia ya watu 1590 waliojeruhiwa kwenye vita mjini Moghadishu 735 ni watoto.

WHO inasema watoto wengi wanaojeruhiwa ni kutokana na kushika kasi kwa mapigano kwenye soko la Barakat ambalo liko kwwenye eneo linalokaliwa na watu wengi.

Watoto wengi wanaolazwa hospitali wameelezwa kuwa na majeraha ya kuungua moto na majeraha kifuani yanyokanayo na milipuko na makombora.

WHO inasema tangu Januari mwaka huu majeruhi 3900 wametibiwa , sasa inatoa mafunzo kwa madaktari na wauguzi kutibu watoto hao kama anavyofafanua DR Tarik Jasarevic wa shirika hilo.

(SAUTI YA DR TARIK JASAREVIC)

Pia WHO imerejea ombi la msaada kwani iliomba dola milioni 58 kwa ajili ya kusaidia Somalia na hadi sasa imepokea dola milioni 9.4 pekee.