Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa dunia waongeza juhudi kukabili ukimwi:UNAIDS

Viongozi wa dunia waongeza juhudi kukabili ukimwi:UNAIDS

Wakati vita vya ukimwi vikiwa katika kiwango cha juu viongozi wa dunia wanaonyesha nia ya kuongeza bidii katika vita hivyo umesema Umoja wa Mataifa.

Zaidi ya Maraisa na makamu wa Rais 30mwa serikali mbalimbali wanajiandaa kukutana kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa wiki ijayo hapa New York kujadili masuala ya ukimwi limesema shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na ukimwi UNAIDS.

Mkutano huo utafanyika wakati ambapo idadi ya watu wnaoishi na virusi vya HIV ni kubwa kuliko wakati mwingine wowowte huku msaada wa kukabiliana na ugonjwa huo ukipungua imesema UNAIDS.

Viongozi hao , mawaziti na wawakilishi kutoka nchi zingine wanachama watakunata kuanzia juni 8 hadi 10 ili kuafikia njia nyingine mpya za kupambana na ukimwi katika jitihada za kufikia malengo ya maendeleo ya milenia hapo 2015 amesema Michel Sidibe mkurugenzi mkuu wa UNAIDS.