Skip to main content

Uhalifu ulifanyika nchini Sri Lanka:HYNES

Uhalifu ulifanyika nchini Sri Lanka:HYNES

 

Mtaalamu wa masuala ya haki za kibinadamu wa Umoja wa Mataifa anasema kuwa anaamini uhalifu mkubwa ulitendeka wakati wa mwisho mwisho wa mapigano nchini Sri Lanka. 

Christof Hynes mjumbe maalum anayeshughulikia mauaji kinyume na sheria anasema kuwa anamiliki kanda za video zinazoonyesha watu waliojihami wakiwaua raia zilizo naswa nyakati za mwisho wa mapigano hayo. Akiwasilisha ripoti yake ya kila mwaka mbele ya baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geveva Bwana Hynes amesema kuwa serikali ya Sri Lanka haijatoa ushahidi baada ya uchunguzi huru kuhusu kile kinachoonekana kama uhalifu.