Naibu katibu mkuu wa UM ahudhuria mkutano wa wanawake viongozi nchini Israel.

30 Mei 2011

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Asha-Rose Migiro alihudhuria mkutano wa wanawake vingozi mwishoni mwa juma kwenye mji wa Haifa nchini Israel ambapo alialikwa kama mgeni wa heshima.

Bi Migiro amekuwa kwenye mstari wa mbele katika kuunga mkono kuinuka kwa wanawake na kuwepo usawa wa kijinsia na pia kuongoza hamasisho wa mwanamke kama ajenti wa maendeleo. Mkutano huo uliondaliwea kwa ushirikiano kati ya serikali ya Israel na shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO liliangazia suala la wanawake, sayansi na teknolojia.

Kisha Bi Migiro alisafiri kwenda mji wa Jerusalem ambapo  alifanya mazungumzo na maafisa wa serikali akiwemo rais Shimon Peres na spika Reuven Rivlin

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter