Mashtaka dhidi ya washukiwa wa uhalifu wa kivita lazima yahusishe ubakaji

30 Mei 2011

Afisa wa ngazi ya juu kwenye Umoja wa Mataifa amesema kuwa washukiwa wawili wa uhalifu wa kivita waliokamatwa kwa kuhusika kwenye uhalifu katika eneo la Balkans na nchini Rwanda ni lazima wakabiliana na mashtaka ya dhuluma za kingono yaliyo mbele yao.

Ratko Madic alikamatwa nchini Serbian wiki iliyopita baada ya kukwepa kukamatwa kwa muda wa miaka 16 huku Bernard Munyagishari akimatawa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud