Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO na taasisi ya Max Planck kufanya uchunguzi wa maradhi yanaoathiri familia tofauti za wanyama na binadamu

FAO na taasisi ya Max Planck kufanya uchunguzi wa maradhi yanaoathiri familia tofauti za wanyama na binadamu

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO na taasisi ya Max Planck nchini Ujerumani wameungana kwenye utafiti wa maradhi Fulani ambayo huwaambubika wanyapori, wale wanaofugwa na hata binadamu.

Kutokana na kupanuka kwa biashara ya wanyama na bidhaa za wanyama hali hi imechangia kusambaa kwa magonjwa yajulikanayo kama zoonoses, magonwa yanayoathiri familia nyingi za wanyama na yaliyo na athahari kubwa kwa wakulima na kwa afya ya binadamu yakiwemo H1N1 na H5N1.

Maafikiano yaliyotiwa sahihi kati ya FAO na taasisi Max Planck yana lengo la kuleta pamoja utaalamu wa pande hizo mbili kushughulikia tatizo hili. Lengo kuu la ushirikiano huo litakuwa ni kubani ni maeneo yapi yako kwenye hatari kwa maambukizi ya maradhi kwa wanadamu , mifugo na wanyamapori.