Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viwango vya gesi chafu duniani vinaongezeka: Figueres

Viwango vya gesi chafu duniani vinaongezeka: Figueres

Makadirio ya hivi majuzi kutoka shirika la nishati duniani IEA yanaonyesha kuwa gesi zinazochafua mazingira ziliongezeka zaidi mwaka 2010 na limetoa onyo kwa serikali kuiga hatua mwaka huu katika kupata suluhu za mabadiliko ya hali ya hewa. Hii ni kulingana na mkuu wa masuala ya hali ya hewa kwenye Umoja wa Mataifa Christiana Figueres ambaye pia amesema kuwa hatua za kimataifa zinastahili kuchukuliwa ili kukabiliana na suala hili.

Wiki ijayo serikali zinakutana mjini Bonn nchini Ujerumani kujiandaa kwa mkutano mkuu kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa utakaoandaliwa mjini Durban mwishoni mwa mwaka huu. Maureen Koech na taarifa kamili.

(SAUTI YA MAUREEN KOECH)