Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay azungumzia dhuluma dhidi ya makundi yanayoipinga serikali nchini Syria na Libya.

Pillay azungumzia dhuluma dhidi ya makundi yanayoipinga serikali nchini Syria na Libya.

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navy Pillay amesema kuwa mbinu zinazotumiwa kukabiliana na waandamanaji wanaoipinga serikali nchini Lybia , Bahrain , Yemen na Syria ni ukiukaji wa haki za binadamu. Akihutubia baraza la haki za binadamu mjini Geneva Pillay amesema kuwa matumizi ya nguvu dhidi ya wanaondamana kwa amani ni kama kuchochea ghasia zaidi. Pillay amesema kuwa dhuluma haziwezi kuzima matarajio ya watu ambao wanaitisha haki zao.

(SAUTI YA NAVI PILLAY)

“Jibu sahihi ni kwa utawala kufanya mazungumzo ili kujishughulisha na matakwa ya wandamaji. Hatua za kwanza zilizochokuliwa na nchi fulani katika kushughulikia matakwa yakiwemo mabadiliko ni lazima zifanyike. Lengo litakuwa kuchukua hatua juu ya masuala kadhaa yaliyowaleta watu mitaani”