UNESCO yazungumzia mahitaji ya vituo vya utangazaji vya kimataifa nchini Misri na Tunisia

30 Mei 2011

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO kwa ushirikiano na kituoa cha runinga nchini Ufaransa pamoja na muungano wa vituo vya utangazaji nchini ulaya wameandaa mkutano ulio na lengo la kuviinua vituo vya utangazi nchini Msiri na Tunisia.

Hii ni baada ya kubainika kuwa mabadiliko kwenye demokrasia nchini Misri na Tunisia yanaweza tu kufanikiwa iwapo yataruhusu kuwepo mazingira bora kwa vyombo vya utangazaji ambapo zaidi ya familia tisini zinamiliki runinga. Wanasema kuwa vyombo vya utangazaji ni muhimu katika kufungua majadiliano, kudumisha imani ya wananchi na kuwawezesha kushiriki katika masuala ya umma. Mapendekezo yatakayotolewa kwenye mkutano huo yatawasilishwa pamoja na hatua ambazo zitachukuliwa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter