Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa lishe ya kutosha kwa watoto kushughulikiwa na wataalamu wa kimataifa

Ukosefu wa lishe ya kutosha kwa watoto kushughulikiwa na wataalamu wa kimataifa

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa zaidi ya watoto milioni 100 walio chini ya miaka mitano wana uzito kidogo , zaidi ya milioni 170 hawakui huku milioni 43 wakiwa na uzito kupita kiasi mwaka 2010.

Kulingana na ripoti kuhusu lishe kwa watoto ni kuwa kuna mpango uliobuniwa ili kukabiliana na suala la ukosefu wa lishe na uzito kupita kiasi. Dr. Francesco Branca afisa kutoka idara ya WHO inayohusika na masuala ya lishe kwa afya na maendeleo anasema kuwa idadi.

(SAUTI YA Dr. Francesco Branca)

kubwa ya watoto bado wanasumbuliwa na ukosefu wa lishe kote duniani. Hatua zinazohitajika zilijadiliwa kwenye mkutano wa baraza wa 64 wa afya duniani ulioandaliwa mjini Geneva kati ya tarehe 16 na 24 mwezi huu.