Ban akaribisha hatua ya kurefushiwa muda baraza la katiba Nepal

Ban akaribisha hatua ya kurefushiwa muda baraza la katiba Nepal

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha hatua iliyochukuliwa na Nepal ya kuliongezea muda baraza la katiba la nchi hiyo ambalo lilipewa jukumu la kupitisha katiba mpya ifakapo mwishoni mwa mwezi huu.

Taifa hilo lililopo Kusini mwa Asia lipo kwenye mchakato wa mwisho kuamsha matumaini ya amani na utulivu kufuatia kipindi kirefu cha vita kilichohusisha vikosi vya serikali na kundi la Maoists. Baraza hilo la Katiba kwa sasa limerefushiwa muda na kupewa kipindi kingine cha

miezi mitatu ili kukamilisha baadhi ya vipengele kabla ya kuidhinishwa rasmi kwa katiba hiyo. Pamoja na kutoa pongezi zake, Ban ametaka pande zinazoshughulia marekebisho hayo kuwajibika ipasavyo  ili hatimaye kuleta matumaini mapya ya amani kwa wananchi

wa Nepal