Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yafungua ofisi yake Mexico ili kuwasaidia wahamiaji

IOM yafungua ofisi yake Mexico ili kuwasaidia wahamiaji

Shirika la Umoja wa Mataifa IOM limefungua ofisi yake katika mji wa Tuxtla uliopo katika jimbo la Chiapas nchini Mexico ambayo itasaidia kuumarisha mahusiano mema na mamlaka za eneo hilo.

Ofisi hiyo pamoja na mambo mengine pia inatazamiwa kushughulikia makundi ya wahamiaji wanaoendelea kuingi kwenye eneo hilo. Eneo la Chiapa, ni lango kuu linalotumiwa na wahamiaji wengi kutokana Amerika ya Kati, China na India kuingia Mexico kwa shabaya ya kuelekea nchini Marekani.

Ofisi hiyo pia inatazamiwa kuendelea kufanya kazi bega kwa bega na mamlaka za Mexico ili kukabiliana na wimbi hilo la wahamiaji.