Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya hofu ya maisha yao, vijana walemavu wa ngozi TZ wa ndoto kubwa za baadaye

Licha ya hofu ya maisha yao, vijana walemavu wa ngozi TZ wa ndoto kubwa za baadaye

Umoja wa Mataifa moja ya misingi yake ni kuzichagiza nchi zote wanachama kuhakikisha zinafuata haki za binadamu kwa watu wake bila ubaguzi wa aina yotote ile.

Kwa mujibu wa mkataba wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa mauaji ya aina yoyote ile yanayofuata misingi ya kabila, rangi, au tabka Fulani yanakwenda kinyume na haki za binadamu za kiamtaifa na kitaifa na wahusika wanapaswa kuchukuliwa hatua kwa uhalifu huo.

Nchini Tanzania walemavu wa ngozi yaani albino wamekuwa wakiishi kwa hofu kwa miaka kadhaa sasa wakihofia kuuawa, au kukatwa viungo vyao ambavyo vinatumiwa kwa misingi ya ushirikina.

Serikali ya nchi hiyo kwa ushirikiano na wananchi imekuwa ikiwasaka na kuwafikisha mbele ya sheria wanaotekeleza ukiukaji huo wa haki za binadamu za kuishi.

Mwandishi wetu wa Dar es salaam George Njogopa amefunga safari hadi Kaskazini Magharibi mwa Tanzania ambako mauaji ya walemavu hao wa ngozi yapo kwa kiasi kikubwa na kuzunguza na baadhi yao. Sikiliza makala hii.

(MAKALA NA GEORGE NJOGOPA)