Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujerumani yachunguza ugonjwa unaoathiri figo)

Ujerumani yachunguza ugonjwa unaoathiri figo)

Mkurupuko wa ugonjwa unaoathiri figo au haemolytic uraemic syndrome unaendelea kuzua wasiwasi nchini Ujerumani baada ya wanawake 3 kuaga dunia na visa 276 vya ugonjwa huo kuripotiwa tangu mapema mwezi huu.

Watu wengine wamelazwa hospitalini wengi wakiwa mahututi huku visa zaidi vikiendekea kuripotiwa. Nchi zingine kama Sweden nazo zimeripoti visa kumi huku wagonjwa wawili wakiwa katika hali mahututi. Wote wanaogua walikuwa wameitembelea ujerumani hasa kaskazini mwa nchi. Shirika la fya duniani WHO linaendelea kutoa usaidizi na linasema kuwa liko tayari kuzisaidia nchi ambazo hazina uwezo wa kutambua ugonjwa huo.