Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mipango ya kurejea nyumbani kwa wakimbizi nchini Chad yaanza

Mipango ya kurejea nyumbani kwa wakimbizi nchini Chad yaanza

 

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeanza kuwasaidia wakimbizi wa ndani kwenye eneo la mashariki mwa Chad kurejea makwao kufuatia kuimarika kwa usalama. Wengi wa wakimbizi walikimbia mapigano ya kikabila kati ya mwaka 2005 na 2006 wakati ghasia ziliposambaa kutoka jimbo ambalo taYari linakumbwa na mzozo la Darfur ambapo vijiji viliteketezwa na mazao mashambani kuharibiwa.

Hata hivyo hadi sasa zaidi ya raia 14,000 wa chad kati ya 130,000 waliokimbia makwao wamejiandikisha kurudi makwao. Pia tangu mwaka uliopita watu 50,000 wamerejea makwao kwa hiyari. Hata hivyo baadhi ya wakimbizi wa ndani hawaonyeshi nia ya kurudi nyumbani wakisema kuwa ni bora waelekee kwingine.