IOM kuonyesha filamu inayooesha hatari za uhamiaji haramu miongoni mwa watoto.

27 Mei 2011

Filamu iliyoundwa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM iliyo na lengo la kutoa hamasisho kuhusu hatari ya kuhama kusiofuata sheria miongoni mwa watoto nchini Misri walio na nia ya kuingia nchini Italia itaonyeshwa tarehe 30 mwezi huu mjini Cairo kama moja ya njia ya kuunga mkono uhamiaji unaofuata sheria.

Filamu hiyo ijukanayo kama “Barabara kuelekea Atalia” itaonyeshwa mbele ya watu 100 kutoka sekta za serikali na za kibinafsi, yakiwemo mashirika ya kimataifa , mawaziri wa serikali na mabalozi. Ikingazia hadithi ya familia kutoka Misri iliyowapoteza watoto watatu wa kiume katika juhudi zao za kuingia Italia kwa bahari wakiwatumia wale wanaowasafirisha kiharamu watu  filamu hiyo inaonyesha hatari nyingi zinazowakumba watoto safarini na wanapowasili salama.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter