Walinda amani wa UNFIL wajeruhiwa Lebanon

27 Mei 2011

Mlipuko wa Bomu umejeruhi walinda amani wa Umoja wa Mataifa walipokuwa kwenye msafara Kusini mwa Lebanon. Kwa mujibu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNFIL ,mlipuko huo umetokea kilometa 40 Kusini mwa mji mkuu Beirut. Andrea Tenenti naibu msemaji wa UNIFIL anasema timu imetumwa kwenye eneo la tukio kuchunguza.

(SAUTI YA ANDREA TENENTI)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikli shambulio hilo la walinda amani na kuongeza kwamba inasikitisha zaidi kwamba limetokea leo ambapo Umoja wa mataifa umefanya hafla maalumu kuwaenzi wanawake na wanaume ambao ni walinda amani wanaoweka maisha yao hatarini kusaidia wengine.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter