Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya walinda amani, msisitizo ni sheria na utulivu

Siku ya walinda amani, msisitizo ni sheria na utulivu

Leo hafla maalumu imefanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York zikiongozwa na naibu Katibu Mkuu Asha- Rose Migiro kuwakumbuka walinda amani wote waliopoteza maisha yao katika juhudi za kuleta amani.

Mai 29 kila mwaka huadhimishwa siku ya kimataifa ya walinda amani na mwaka huu kauli mbiu ni kuimarisha utawala wa sheria .

Katika ujumbe maalumu wa siku hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema anawaenzi zaidi ya wanajeshi, polisi na raia 120,000 wanaofanya kazi katika mipango mbalimbali ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa duniani na kuwaenzi wale waliopoteza maisha yao kwa ajili ya kupigania amani yaw engine.

Amesema kuadhimisha siku hii kunamaanisha kwamba wale walionusurika vita hawastahili kuteseka tena kwa kutokupata haki, kuwa na usalama na woga na bila kuonda vikwazo hivi amani itaendelea kuwa hatarini.

 Amesisitiza umuhimu wa juhudi za walinda amani katika kuhakikisha utawala wa sheria unadumishwa, na hata wengine wamepoteza maisha yao akitaja jumla ya walinda amani zaidi ya 173 waliopoteza maisha kati ya mwaka 2010 na mwaka huu kutokana na majanga ya asili, kama Haiti, ghasia, ajali na magonjwa wakiwa kazini.

Amesema wakati tukiwakumbuka waliokufa lazima pia tuenzi kazi yao. Miongoni mwa wanaohusika na masuala hayo ya kulinda amani ni Jairus Omondi ambaye ni afisa wa Magereza Darfur Sudan:

(SAUTI YA JAIRUS OMONDI)