27 Mei 2011

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ameshiriki mjadala kuhusu matukio yanayoendelea Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati,  kanda ya Afrika kwa ujumla na masuala ya maendeleo.

Mjadala huo umefanyika mjini Deauville nchini Ufaransa ambako vigogo wa nchi nane tajiri duniani G-8 wanakutana.

Kuhusu Afrika ya Kaskazini na Mashariki ya Kati Ban amesisitiza kwamba jumuiya ya kimataifa lazima ishikamane na kuchukua hatua pamoja na kuwasiliana kwa mpango maalumu.

Pia metaka msaada wa kibinadamu uongezwe kwa watu wa Libya na jirani zao. Ameongeza kuwa ajira na fursa za elimu kwa vijana na wanawake ni muhimu sana.

Anmezungumzia pia mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati na kutaka jumuiya ya kimataifa kushirikiana kusukuma mbele juhudi hizo. Na kuhusu matatizo ya kwingineko afrika ameongelea hali ya Ivory Coast, Somalia na Sudan ambako amesema juhudi zaidi zinahitajika kuhakikisha amani na usalama wa kudumu unapatikana.

Masuala mengine aliyogusia ni afya kwa kina mama na watoto, usalama wa chakula, nishati, maendeleo , mabadiliko ya hali ya hewa na mkutano wa Rio mwaka 2012.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter