Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji bado wanakabiliwa na adha Libya:UNHCR

Wahamiaji bado wanakabiliwa na adha Libya:UNHCR

Shirika la kuhudumiaa wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema wiki hii umeshuhudia usumbufu na ghasia kubwa kwenye kambi ya Choucha karibu na mpaka wa Tunisia na Libya ambako wafanyakazi wahamiaji karibu 4000 na wanaokimbia machafuko Libya wanahifadhiwa.

Watu hao wanasubiri kuhamishwa kupelekwa ama makwao au kwenye usalama zaidi. Raia wanne wa Eritrea wamekufa kambini hapo baada ya moto kuzuka wakati wahamiaji hao wakiwa wamelala.

Moto huo uliteketeza kabisa mahema 20 na chanzo chake bado kinachunguzwa. Kambi hiyo ilikuwa na watu 4500 wakati huo wengi wakiwa ni Wasomali, Waeritrea na Wasudan.

Na matatizo yameendelea baada ya kundi kubwa la wahamiaji kuzingira ofisi za UNHCR wakitaka kupatiwa makazi maramoja. Melissa Fleming ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA MELISSA FLEMING)