Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kipindupindu hakijaisha Haiti:WHO

Kipindupindu hakijaisha Haiti:WHO

Shirika la afya duniani WHO limesema kipindupindu kinasalia kuwa tishio kubwa kwa jamii nchini Haiti miezi saba tangu kilipozuka. Hadi kufikia leo watu takribani 5000 wamekufa kwa ugonjwa huo Haiti, huku visa zaidi ya 290,000 vikiripotiwa.

WHO inasema ingawa juhudi kubwa zimefanyika kudhibiti ugonjwa huo, maeneo mengine yanayoathirika yanaendelea kuibuka, la karibuni kabisa likiwa wilaya ya Magharibi.

WHO inasema msaada wa dharura wa tiba ya kipindupindu umepelekwa kwenye maeneo yaliyoathirika ili kutibu na kuzuia usirejee tena Pourt-au-Prince, kama anavyosema Fadela Chaib wa WHO

(SAUTI YA FADELA CHAIB)