Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa dunia waunga mkono elimu kwa wasichana

Viongozi wa dunia waunga mkono elimu kwa wasichana

 

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton, waziri mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina pamoja na waziri mkuu wa Mali Cissé Mariam Kaïdama Sidibé wameungana na viongozi wengine kutoka kote duniani kwenye uzinduzi wa mpango wa kuunga mkono elimu ya wanawake mjini Paris.

Wasichana milioni 39 kutoka kote duniani walio na umri wa kuwa wanafunzi kwenye shule za upili kwa sasa hawajajiunga na masomo ya msingi wala ya upili kote duniani huku thuluthi mbili ya watu milioni 796 wasiojua kusoma wala kuandika wakiwa ni wanawake.