Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali bado tete huku maelfu wakikimbia Abyei:OCHA

Hali bado tete huku maelfu wakikimbia Abyei:OCHA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema kuwa maelfu ya watu waliokimbia eneo la Abyei nchini Sudan wamewasili kwenye sehemu zilizo kaskazini mwa Sudan Kusini.

Hata hivyo haijabainika idadi kamili ya waliokuwa wenyeji 110,000 wa eneo la Abyei waliokimbia makwao. Usambazaji wa chakula kwa watu 3000 umeanza katika eneo la Mayen Abun kwenye jimbo la Warrap.

Hali inasalia kuwa tete huku uporaji wa mali ukiripotiwa kwenye mji wa Abyei kulingana na vile msemaji wa OCHA Elisabeth Byrs anavyoeleza.

(SAUTI YA ELIZABETH BYRS)