Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ramani mpya ya maji Afrika yazinduliwa

Ramani mpya ya maji Afrika yazinduliwa

Ramani inayoonyesha picha mwafaka kuhusu maeneo ya maji kote barani Afrika imezinduliwa na shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP. Ramani hiyo iliyozinduliwa wakati wa maadhimiso ya siku ya Afrika ina picha 100 za satellite , Ramani 222 na ishara 500.

Mkurugenzi kwenye ofisi inayohusika na kutoa ushuri kuhusu bara la Afrika Patrick Hayford anasema hata baada ya mataifa 26 barani Afrika kupiga hatua katika kuhakikisha kuwepo kwa maji safi ni tisa tu yalizoporesha usafi akiongeza kuwa maji na usafi ni masuala makuu barani Afrika.

(SAUTI YA PATRICK HAYFORD)