Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zichukuliwe kukabili homa ya nguruwe:FAO

Hatua zichukuliwe kukabili homa ya nguruwe:FAO

 

Shirika na la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO limezitaka nchi ambazo tayari zimeathirika na ugonjwa wa nguruwe kwenye eneo la Caucasus na Urusi kuchukua hatua mawafaka ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.

Afisa mkuu wa masuala ya tiba kwa wanyama kwenye shirika la FAO Juan Lubroth anasema kuwa kwa sasa ugonjwa huo umekuwa suala la kimataifa.

 Amesema kuwa ugonjwa wa nguruwe umekuwa hata hatari kubwa barani ulaya na sehemu zingine akiongeza kuwa nchi zinastahili kuwa waangalifu na kujiimarisha katika kujiandaa kukabiliana na ugonjwa huo.