Mapigano mapya yaikumba Yemen

26 Mei 2011

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa anaendelea kusumbuliwa na kuendelea kushuhudiwa kwa ghasia nchini Yemen ambapo maelfu ya watu wamekuwa wakiandamana wakiipinga serikali tangu mapema mwaka huu.

Kupitia kwa msemaji wake Ban anasema kuwa anasambuliwa na makabiliano kwenye mji wa Sanaa kati ya wanajeshi wa serikali na makundi yaliyojihami ambapo watu wengi wameuawa na wengine kujeruhiwa.

Ban anasema kuwa hali hii huenda ikaivuruga nchi hiyo na kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano hayo. Amezitaka pande husika kutafuta njia za kupata suluhu la mzozo wa kisiasa uliopo nchini humo.

Vyombo vya habari vinaripoti kuwa mapigano ya siku tatu kwenye mji wa Sanaa juma hili yamesababisha vifo vya watu 24 huku ripoti zingine zikisema kuwa huenda idadi hiyo ikawa ya juu.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter