Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wasaidia kutoa umeme shuleni Lebanon

UM wasaidia kutoa umeme shuleni Lebanon

Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP linasema kuwa mradi unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kwa sasa unatoa vifaa ya kupokea nishati kutoka kwa jua kwenye shule 25 kusini mwa Lebanon.

Vifaa hivyo vinachukua mahala pa mitambo iliyo yenye gharama kubwa kuendesha kwenye miji iliyoharibiwa mwaka 2006 wakati wa vita na Israel.

Sehemu zingine 36 kote nchini Lebanon zikiwemo shule saba zinatarajiwa kupata vifaa hivyo kwa gharama ya dola milioni 10 kwenye mradi ulioanzishwa mwaka 2007 na Lebanon, Hispania na UNDP.

Majengo mengi ya umma nchini Lebanon pamoja na shule hukumbana na matatizo ya kupotea kwa umeme ambayo hudumu hadi masaa sita kurekebishwa.

Hii ni sehemu ya mradi wa UNDP kuisadia nchi hiyo baada ya uharibifu uliosababishwa na mzozo wa mwaka 2006.