Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujumbe wa IMF wakamilisha ziara nchini Kenya

Ujumbe wa IMF wakamilisha ziara nchini Kenya

Ujumbe kutoka shirika la fedha duniani IMF uliokuwa ziarani mjini Nairobi Kenya chini ya uongozi wa Domenico Fanizza tangu tarehe 11 mwezi huu umekamilisha ziara yake.

Ukiwa nchini Kenya ujumbe huo ulikutana na waziri mkuu , naibu waziri mkuu, Gavana wa benki kuu na maafisa wengine wa ngazi za juu serikalini.

Wakati wa kukamilika kwa ziara hiyo bwana Faniza amesema kuwa programu za mabadiliko ya kiuchumi nchini zimeanza kwa njia nzuri akiongeza kuuwa mafanikio katika sekta ya kilimo na sekta za kibinafsi zimesaidia kuinuka kwa uchumi.

Ujumbe huo uliishauri serikali ya Kenya kutekeleza programu zenye manufaa ili kupata kukua kuambatana na maendeleo ya malengo ya milenia. Hata hivyo ujumbe huo ulisema kuwa uhaba wa mvua ni hatari kwa uchumi suala ambalo linastahili kushughulikwa kwa haraka.