Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Africa, Ban aeleza hatua zilizopigwa kuboresha afya ya mama na mtoto

Africa, Ban aeleza hatua zilizopigwa kuboresha afya ya mama na mtoto

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa ziarani Ethiopia amezuru mpango wa afya vijijini ambao unatoa mafunzo kwa wasichana ya jinsi ya kunusuru jamii zao. Mahitaji ya huduma za afya nchini Ethiopia ni makubwa na yanachukuliwa kama mfano barani Afrika.

Ban pia amekutana na wanawake na watoto katika nyumba zao, katika vituo vya afya na hospitali ili kushuhudia hali halisi na kubaini changamoto zinazowakabili katika kufikia malengo ya afya kwa kila mwanamke na kila mtoto.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye kituo cha afya cha Ambo Mesk Ban amesema wataboresha programu za afya na kupanua wigo wake Ethiopia ambako inaelezwa kwamba kila dakika 25 mwanamke anafariki dunia kutokana na matatizo ya afya, hivyo mpango huo utasaidia kuokoa maisha ya mamilioni ya watu.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Baadaye jioni ya leo Ban atahudhuria mkutano wa Muungano wa Afrika ambao umeaanza leo mjini Addis Ababa kujadili suala la Libya na Ivoy Coast.