Kuwawezesha vijana kwa maendeleo kauli katika siku ya Afrika

25 Mei 2011

Leo ni siku ya Afrika ambayo mwaka huu kauli mbiu ni kuwawezesha vijana kwa ajili ya maendeleo endelevu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anaadhimisha siku hii kwa kuzuru bara hilo kwa lengo la kuchagiza juhudi za kimataifa kupunguza vifo vya kina mama na watoto.

Katika ujumbe maalumu Ban amesema juhudi zinakwenda polepole katika lengo hilo ikilinganishwa na melengo mengine ya maendeleo ya milenia licha ya kuimarisha sera, huduma na teknolojia.

Pia amegusia ukweli kwamba bara la Afrika limeshuhudia muongo wa kukua kwa uchumi haraka, huku nchi zilizo kinara ni zile za kusini mwa Jangwa la sahara na zikishuhudia pia fursa nyingi za uwekezaji.

Amelitaka bara hizo kuendelea kuongeza bidii ili kutokomeza umasikini, na kuleta amani ya kudumu kwenye migogoro.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter