Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

40,000 wakimbia machafuko Abyei Sudan:UM

40,000 wakimbia machafuko Abyei Sudan:UM

Machafuko yanayoendelea katika jimbo lonalogombewa la Abyei Sudan yamesababisha watu takriban 40,000 kuzikimbia nyumba zao , huku kukiwa na taarifa za uhalifu wa kivita, uporaji na kuchoma moto nyumba umesema Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa mpango wa Umoja wa Mataifa Sudan UNMIS idadi ya watu wanaokimbia ghasia imeongezeka. Awali ilikisiwa watu kati ya 20,000 na 30,000 ndio waliokimbia mapigano.

Idadi hiyo ni pamoja na 10,000 ni wanaokimbia mapigano ya moja kwa moja eneo la Abyei na wengine 25,000 ni kutoka eneo la Agok kwenye mpaka wa Sudan Kusini ambako watu wanazihama nyumba zao wakihofia machafuko zaidi siku za usoni.

Msemaji wa UNMIS Kouider Zerrouk aliyewasili Abyei anaeleza hali aliyoishuhudia.

(SAUTI YA KOUIDER ZERROUK)